Masaki Wellspring Hub (MWH), kwa kushirikiana na Mradi wa GenZERO Sickle Cell 2050 wa Ruge Mutahaba Foundation, imeandaa Maonyesho ya Afya Masaki 2026 yatakayofanyika Jumapili, Septemba 27, Masaki jijini Dar es Salaam, yakilenga kuongeza uelewa kuhusu ugonjwa wa selimundu na kuhamasisha upimaji wa mapema.
Jumanne, Septemba 22, 2026

Dar es Salaam. Masaki Wellspring Hub (MWH), kwa kushirikiana na Mradi wa GenZERO Sickle Cell 2050 wa Ruge Mutahaba Foundation, imeandaa Maonyesho ya Afya Masaki 2026 yatakayofanyika Jumapili, Septemba 27, Masaki jijini Dar es Salaam, yakilenga kuongeza uelewa kuhusu ugonjwa wa selimundu na kuhamasisha upimaji wa mapema.
Maonyesho hayo yataanza kwa mbio na matembezi ya jamii, yakifuatiwa na shughuli za afya na ustawi zitakazowezesha wananchi kupata huduma mbalimbali, ikiwamo uchunguzi wa afya bila malipo, ushauri wa kinasaba, ukaguzi wa hali ya afya na taarifa kuhusu huduma za afya.
Uhamasishaji kuhusu selimundu utakuwa sehemu kuu ya shughuli hizo zinazofanyika katika mwezi wa uhamasishaji kuhusu selimundu.
Akizungumza leo Jumanne, Septemba 22, 2026, kuelekea tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa MWH, Dk Yonazi Charles, amesema ugonjwa wa selimundu unaendelea kuwa changamoto kiafya kutokana na uelewa mdogo, dhana potofu, unyanyapaa na mwitikio mdogo katika upimaji wa mapema.
Amesema mpango huo unalenga kuhamasisha watu kufahamu hali zao za kiafya na kuchukua hatua kwa kuzingatia taarifa sahihi.
“Ujumbe wa maonyesho haya ni ‘Pima, Jua, Chukua Hatua.’ Tunataka watu waelewe kwamba kufahamu hali yao kuhusu selimundu kunaweza kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi kwa ajili yao wenyewe na familia zao,” amesema Dk Charles.
Amesema uchunguzi wa afya uliofanywa hivi karibuni na MWH katika jamii ulibaini kuwa asilimia 13.6 ya waliopimwa walikuwa wabebaji wa vinasaba vya selimundu, huku wengi wao wakiwa hawakujua hali hiyo hapo awali.
Dk Charles amesema matokeo hayo yanaonesha umuhimu wa kusogeza huduma za uhamasishaji na upimaji karibu na jamii, hasa vijana na familia.
Maonyesho hayo yatakayoshirikisha waonyeshaji zaidi ya 20, yatahusisha uchangiaji damu, huduma za afya ya akili na msaada wa kisaikolojia na kijamii, huduma zinazohusiana na selimundu pamoja na eneo maalumu kwa watoto.
Mkurugenzi Mtendaji wa Ruge Mutahaba Foundation, Elias Tryphone amesema afya ni miongoni mwa maeneo muhimu ya msingi ya taasisi hiyo, huku uhamasishaji kuhusu selimundu ukiwa sehemu ya ajenda yake.
Amesema taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Afya kuongeza uelewa kuhusu ugonjwa huo, ikilenga zaidi vijana, upimaji wa mapema, kinga na maisha yenye afya.
“Tumekuwa tukihamasisha kuongeza uelewa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, tukilenga zaidi vijana, upimaji wa mapema, kinga na maisha yenye afya kwa ajili ya maisha marefu na yenye afya zaidi,” amesema Tryphone.
Ameongeza kuwa ushirikiano na MWH unalenga kuunganisha nguvu ili kuwafikia watu wengi zaidi, huku akizitaka taasisi na mashirika mengine kuunga mkono juhudi hizo.
Mwenyekiti wa Bodi ya MWH, Fortunatus Ekklesiah amesema mpango huo haujalenga kuwa tukio la siku moja pekee, bali pia kuzikutanisha jamii, kuboresha upatikanaji wa taarifa na huduma za afya na kuhamasisha watu kuwajibika kwa kufahamu hali zao za kiafya.
Maonyesho hayo yanaendeleza tukio la mwaka 2025 lililowakutanisha washiriki 532 na waonyeshaji 21. Katika tukio hilo, watu 158 walipatiwa ushauri, huku 81 wakipimwa kuhusu hali ya kuwa wabebaji wa vinasaba vya selimundu.
MWH imesema inalenga kutumia mafanikio hayo kama msingi wa maandalizi ya Maonyesho ya Marathon ya Masaki na Afya yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2027.
Waandaaji wamewaalika wananchi, wataalamu wa afya, mashirika ya kijamii na wadau wengine kushiriki katika maonyesho hayo kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu selimundu, kuhamasisha upimaji wa mapema na kuhimiza jamii kuishi maisha yenye afya.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Mbeya yaweka mikakati kudhibiti ugonjwa wa seli mundu | 0 | 8.36 | 21-09-2026 |
| 2 | The date of Friendship Cup-2026 announced | 0 | 12.74 | 10-06-2026 |
| 3 | На пересечении международных маршрутов и новых технологий:TransLogistica Kazakhstan 2026 соберет в Астане лидеров транспортно-логистической отрасли | 0 | 18.72 | 21-09-2026 |
| 4 | Celle Drilling 2026 - The Way Ahead | 0 | 14.93 | 15-09-2026 |
| 5 | קריקטורה יומית | 14 באוגוסט 2026 | 0 | 50 | 13-08-2026 |
| 6 | Translogistica Kazakhstan 2026 в активной фазе подготовки: 80% выставочной площади уже забронировано, регистрация посетителей открыта | 0 | 26.74 | 30-07-2026 |
| 7 | קריקטורה יומית | 13 באוגוסט 2026 | 0 | 50 | 12-08-2026 |
| 8 | 「2026 High School Festival」を開催します【令和8年9月6日】 | 0 | 19.53 | 01-08-2026 |
| 9 | קריקטורה יומית | 9 ביולי 2026 | 0 | 0 | 08-07-2026 |
| 10 | Ōku Wāhi I My Places – Exhibition | 0 | 16.38 | 21-08-2026 |