Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Wanaouza dawa za meno kwenye mabasi, mitandaoni hii inawahusu

Дата публикации: 20-09-2026 12:13:28

Wizara ya Afya imeonya watu wanaotumia mabasi ya masafa marefu na mitandao ya kijamii kuuza dawa za meno kwa madai ya kutibu yaliyooza, kutoboka au kuyafanya meupe, ikisema biashara hiyo inaweza kupotosha wananchi na kuchelewesha matibabu sahihi.

Основное содержимое страницы с новостью.

Jumapili, Septemba 20, 2026

Muktasari:
  • Wizara ya Afya yasema bidhaa zinazodaiwa kutibu meno yaliyooza na kuyafanya meupe zinaweza kuchelewesha matibabu na kusababisha madhara

Dar es Salaam. Wizara ya Afya imeonya watu wanaotumia mabasi ya masafa marefu na mitandao ya kijamii kuuza dawa za meno kwa madai ya kutibu yaliyooza, kutoboka au kuyafanya meupe, ikisema biashara hiyo inaweza kupotosha wananchi na kuchelewesha matibabu sahihi.

Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Kinywa na Meno wa Wizara ya Afya, Dk Baraka Nzobo, amesema watu wasio na taaluma wala leseni za kutoa huduma za kinywa na meno hawapaswi kutumia vyombo vya usafiri au mitandao ya kijamii kutoa huduma au kuuza bidhaa kwa madai ya kutibu matatizo ya meno.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili, Septemba 20, 2026, Dk Nzobo amesema baadhi ya watu wamekuwa wakipanda mabasi yanayosafiri mikoani na kujitambulisha kama wataalamu, kisha kuwaeleza abiria kuhusu dawa wanazodai zina uwezo wa kutibu meno yaliyooza, kutoboka au kuondoa rangi ya kahawia na njano.

Amesema baadhi yao pia wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kutangaza bidhaa hizo, jambo linaloweza kuwafanya wananchi kuamini kuwa, wanaweza kutibu matatizo ya meno bila kufika hospitalini.

“Watu wanaotaka kutoa elimu ya afya ya kinywa na meno kwa jamii wakasomee taaluma hiyo katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, kuanzia ngazi ya stashahada ya utabibu wa kinywa na meno hadi shahada ya udaktari wa kinywa na meno,” amesema.

Maumivu ‘kufichwa’

Dk Nzobo amesema baadhi ya bidhaa zinazodaiwa kupunguza maumivu ya jino zinaweza kumfanya mtumiaji asihisi maumivu kwa muda, wakati chanzo cha tatizo kikiendelea ndani ya jino.

Amesema hali hiyo inaweza kufanya mgonjwa kuchelewa kufika hospitalini na wakati mwingine tatizo kuwa kubwa zaidi.

“Jino linaweza kuendelea kutengeneza usaha kimya kimya ndani ya jino na taya, baadaye mtumiaji anakuja kushtuka shavu limemvimba na kuanza kupata maumivu kutokana na jipu la jino,” amesema.

Dk Nzobo amesema jipu la jino mara nyingi hutokana na jino lililooza kwa muda mrefu bila kupata matibabu, ikiwamo kuondoa sehemu iliyooza na kuliziba au kufanyiwa matibabu ya mzizi wa jino (root canal treatment).

Amesema kuchelewesha matibabu kunaweza kuongeza gharama na kusababisha madhara makubwa zaidi, ikiwamo maambukizi yanayoweza kuathiri mfupa wa taya.

Madai ya kufanya meupe

Kuhusu madai ya baadhi ya wauzaji kwamba dawa zao za meno zinaweza kubadili meno yenye rangi ya kahawia au njano na kuyafanya meupe, Dk Nzobo amesema dawa za kawaida za meno hazina uwezo huo kwa kiwango kinachodaiwa.

Amesema watu wenye meno yaliyobadilika rangi wanapaswa kufika hospitalini kwa uchunguzi na kupata huduma kutoka kwa wataalamu waliobobea katika tiba ya urembo wa meno (Cosmetic Dentistry).

Amesema hali ya kubadilika rangi kwa meno imeonekana zaidi katika baadhi ya maeneo, yakiwamo Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Kondoa, Singida, Shinyanga na Rungwe, ambako kiwango cha fluoride katika maji na vyanzo vingine kinaweza kuwa kikubwa.

“Dawa zote za meno zenye madini ya fluoride kazi yake kubwa ni kuzuia meno yasitoboke na kuyang’arisha. Kukinga meno kuoza na kung’arisha si kutibu au kuyafanya meno kuwa meupe,” amesema.

Amesema jino linapooza au kutoboka, mgonjwa anapaswa kufika hospitalini kwa uchunguzi na kupata matibabu kutoka kwa mtaalamu wa kinywa na meno, badala ya kutegemea bidhaa zinazouzwa mitandaoni au kwenye mabasi.

Mabasi yaonywa

Wizara ya Afya imewataka wamiliki wa mabasi kutoruhusu watu wasio na taaluma na leseni kutoa elimu au kuuza bidhaa zinazohusiana na afya ya kinywa na meno ndani ya vyombo vyao.

Dk Nzobo amesema hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaokiuka agizo hilo, wakiwamo watu wanaotoa taarifa za upotoshaji kuhusu huduma za kinywa na meno pamoja na wamiliki wa vyombo vya usafiri.

Takwimu za meno

Wizara ya Afya imesema asilimia 76.5 ya watu wenye umri wa miaka 15 na kuendelea nchini wana tatizo la kuoza meno, huku asilimia 31.1 ya watoto wakiwa na tatizo hilo kwenye meno ya utotoni.

Mbali na kuoza meno, magonjwa ya fizi yanaendelea kuwa changamoto kwa wananchi, yakikabili asilimia 67 ya watu wazima na asilimia 57 ya watoto, kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya.

Wakati hayo yakibainishwa, utafiti mpya umeonyesha kuwa kijana mmoja kati ya wanane nchini amewahi kupata maumivu ya kinywa ndani ya mwezi mmoja, hali iliyohusishwa na kuongezeka kwa msongo wa mawazo, wasiwasi na kupungua kwa ustawi wa maisha.

Utafiti huo uliwahusisha wanafunzi 1,000 kutoka shule 20 za msingi za Serikali jijini Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani. Ulifanywa na watafiti kutoka Tanzania na Marekani, akiwamo Magreat Somba wa Taasisi ya Afya Ifakara (IHI).

Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa katika jarida la kitaaluma la Community Dental Health, likieleza athari za maumivu ya kinywa kwa ustawi wa watoto na vijana.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Mbeya yaweka mikakati kudhibiti ugonjwa wa seli mundu08.3621-09-2026
2Зубную боль приводят в порядок // Минздрав обязал стоматологов проводить болезненное лечение с анестезией08.5326-08-2026
3Минздрав обяжет стоматологов ставить обезболивание при болезненных процедурах08.2627-08-2026
4Министр баланың тісін емдеуге талон іздеп кеткен ата-аналардың мәселесін шешуді тапсырды015.2615-08-2026
5Минздрав предложил ввести штрафы за перекуры на работе0017-08-2019
6Harufu mbaya inavyogeuka mtego kwa afya -101020-09-2026
7Минздрав предложил включить лекарства в систему, не допускающую продажу "просрочки"0014-03-2023
8Минздрав не намерен требовать внедрения программ по укреплению здоровья на предприятиях0019-08-2019
9Минздрав не обсуждает инициативу увеличения возраста продажи сигарет0019-11-2019

Классификация: Общество. Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 9. Тональность: 0. Информативность: 6.82. Источник: www.mwananchi.co.tz.