Kuna swali ambalo jamii imekuwa ikimuuliza mwanamke mara nyingi kuliko inavyostahili. Swali huwa: “ Je, Umeolewa? Una watoto wangapi?”
Jumapili, Septemba 20, 2026

Picha na Mtandao.
Mwananchi Comminications Ltd
Dar es Salaam. Kuna swali ambalo jamii imekuwa ikimuuliza mwanamke mara nyingi kuliko inavyostahili. Swali huwa: “ Je, Umeolewa? Una watoto wangapi?”
Kwa wengi, maswali haya yanaonekana kuwa ya kawaida. Lakini kwa mwanamke anayesubiri kupata mtoto, ambaye hajaolewa, aliyeachika, mjane au aliyeamua kuchelewa kuingia kwenye ndoa, yanaweza kuwa chanzo cha maumivu na shinikizo.
Katika baaadhi ya jamii, mwanamke amekuwa akitambulishwa kupitia nafasi yake ya kuwa mama. Kuanzia katika familia hadi kwenye jamii, mafanikio ya mwanamke mara nyingi hupimwa kwa uwezo wake wa kuzaa, kulea watoto na kuhakikisha familia inaendelea kuwa na mshikamano.
Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya jamii, mtazamo wa kumuona mwanamke hasa kupitia nafasi yake ya uzazi, unaweza kuficha mchango mkubwa anaoutoa katika maendeleo ya familia na taifa.
Mwanamke ni zaidi ya uzazi
Akizungumza na Mwananchi Digital, mchambuzi wa masuala ya kijamii na mtaalamu wa malezi, Irene Mwakalinga amesema thamani ya mwanamke ni zaidi ya jukumu la malezi.
Mwakalinga amesema kuwa mama ni sehemu muhimu ya maisha ya wanawake, lakini si kipimo pekee cha thamani yao.
Amesema kutokana na baadhi ya watu katika jamii kutolitambua hilo, huiangalia thamani ya mwanamke kutokana na uwezo wa kupata watoto, jambo ambalo kwa mujibu wa Mwakalinga siyo sahihi na linaipotosha jamii.
“Mtazamo huu unaweza kuwaumiza wanawake, ambao kwa sababu mbalimbali, hawajapata watoto au wameamua kutokuwa na watoto. Ukweli ni kwamba utu na thamani ya mwanamke havitokani na uwezo wake wa kuzaa. Mwanamke anapaswa kuheshimiwa kwa misingi ya utu, uwezo, mchango wake na haki zake kama binadamu,”amesema.
Anasema ukiweka kando jukumu la kuwa mama, mwanamke ana mchango katika kukuza uchumi wa familia, jamii na taifa kwa ujumla.
Amesema katika miaka ya hivi karibuni, wanawake wameendelea kushiriki katika shughuli za kiuchumi.
Kuanzia biashara ndogondogo hadi kuinuka na kutengeneza ajira kwa wengine,”amesema.
Anaeleza kuwa pamoja na mwanamke kushiriki katika kukuza uchumi, pia ni kiongozi.
Amesema wanawake wameweza kuonyesha uwezo wao kuanzia katika ngazi ya familia hadi nchi wakitekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
“Wanawake kama ilivyo kwa wanaume wana uwezo wa kufanya uamuzi, kusimamia rasilimali na kushiriki katika kutatua changamoto zinazozikabili jamii,”ameeleza.
Pamoja na nafasi na majukumu mengine ambayo mwanamke amekuwa akiyafanya, bado katika baadhi ya jamii zimeendelea kushikilia dhana kwamba thamani ya mwanamke inaonekana pale atakapoolewa na kufanikiwa kupata watoto.
Nini kifanyike?
Akifafanua hilo mchambuzi wa masuala ya kijamii, Zena Kamonga anasema ili kuondoa dhana hiyo katika jamii, mabadiliko yanatakiwa kuanza katika ngazi ya familia kwa kumuangalia mwanamke katika picha ya zaidi ya kuwa mama.
“Watoto wa kike wanapaswa kukuzwa wakijua kuwa wana uwezo wa kusoma, kufanya kazi, kuanzisha biashara, kuongoza na kufanya uamuzi kuhusu maisha yao, pia watoto wa kiume wakuzwe kuiona thamani ya mwanamke ni zaidi ya kuwa mama,”amesema.
Anaongeza: “Jamii pia inahitaji kubadili lugha na mitazamo inayomdhalilisha mwanamke au kumfanya aonekane kuwa na thamani pale tu anapokuwa mama. Ni muhimu kuelewa kuwa kuwa mama ni jukumu kubwa na lenye heshima, lakini si utambulisho pekee wa mwanamke,”amesema.
Amesema mwanamke anaweza kuwa mhimili wa uchumi kupitia biashara ndogo, ajira au shughuli za uzalishaji na hata kusimama kama viongozi katika jamii.
“Wapo wanawake wanaoendesha biashara, wanalima, wanafanya kazi ofisini na viwandani, huku wengine wakiongoza taasisi na mashirika makubwa, ”amesema.
Kumtazama mwanamke kwa upeo mpana si kupunguza thamani ya umama. Badala yake, ni kutambua kwamba nyuma ya jina “mama” kuna mtu mwenye historia, ndoto, vipaji, uwezo na haki ya kuishi maisha yenye maana.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Familia zinakosea wapi kuacha watoto wa mitaani? | 0 | 8.56 | 20-09-2026 |
| 2 | Mauki: Usifanye haya unapotafuta mchumba | 0 | 9.03 | 20-09-2026 |
| 3 | KCMC: Maumivu makali ya hedhi si ya kupuuzwa | 0 | 5.06 | 20-09-2026 |
| 4 | Чаму многім жанчынам бракуе груднога малака | 0 | 10 | 24-05-2026 |
| 5 | Чыноўнікі пераблыталі нумар кватэры і засялілі жанчыну не туды, а калі яна зрабіла рамонт, запатрабавалі памяняцца з суседам | 0 | 10 | 02-08-2026 |
| 6 | Навукоўцы: жанчыны дасягаюць «крытычнай кропкі» фертыльнасці прыкладна ў 49 гадоў | 0 | 20 | 14-07-2026 |
| 7 | O čemu parovi 'šapuću' nakon seksa? Evo što prvo kažu žene, a što muškarci | 0 | 6.75 | 02-08-2026 |
| 8 | 💬 «Ну назови хотя бы один предмет, который изобрела женщина…» ... | 0 | 2.5 | 06-09-2026 |
| 9 | אם לשבעה וד"ר לפסיכולוגיה: מה באמת חוסם נשים בדרך לקשר | 0 | 9.25 | 26-07-2026 |